KAMISHNA MKUU WA TRA ATOA TUZO YA HESHIMA KWA MATI SUPER BRANDS LTD

0

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda ametoa Tuzo ya heshima kwa Kampuni ya uzalishaji wa vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited kwa kutambua mchango wao katika kulipa kodi stahiki kwa Serikali ambapo kwa kipindi cha miezi mitano Kampuni hiyo imelipa kodi ya shilingi bilioni 5.

Mwenda ametoa Tuzo hiyo alipotembelea kiwanda cha Kampuni hiyo kilichopo Mjini Babati Mkoani Manyara na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji wa vinywaji vyenye ubora unaofanywa katika kiwanda hicho ambapo ameahidi kwamba TRA itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha Kampuni hiyo inakua na kufikia malengo yake.

“Sisi kama TRA tuko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Kampuni ya Mati Super Brands Limited na kuhakikisha tunatatua changamoto zinazowakabili ili iendelee kufanya vizuri zaidi” amesema Mwenda wakati wa ziara yake katika kiwanda cha Mati Super Brands.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo David Mulokozi ameipongeza Mamlaka ya mapato TRA kwa kutoa ushirikiano mkubwa ulioiwezesha Kampuni hiyo kukua kwa kasi na kuongeza kasi ya usambazaji wa bidhaa zake ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Mulokozi amesema kwasasa Kampuni ya Mati Super Brands imeanza kusambaza bidhaa zake katika masoko ya Nchi za Congo, Zambia na Malawi na itaendelea kuzalisha bidhaa bora zenye viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *