KIJIJI CHA NDELENYUMA-MADABA-RUVUMA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MRADI WA MAJI WA BIL.1.6

0

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso leo tarehe 18 Septemba 2024 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Ndelenyuma – Lutukira wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.6 unaotekelezwa na mkandarasi DIMETOCLASA REAL HOPE LIMITED unaotarajiwa kuhudumia wananchi wapatao 4,331 ambao umefikia asilimia 87.5% na maeneo mengine yakianza kupata Maji.

Aidha wananchi wa kijiji hicho wamemshukuru sana Rais Samia kwa mradi huo wa Maji ambao unakwenda kumaliza kabisa changamoto ya Maji.
Akizungumza na wana Ndelenyuma Aweso amemtaka mkandarasi ifikapo mwezi wa 10 mradi huo uwe umekamilika ili wananchi waendelee kupata huduma bora ya majisafi na salama.

Katika hatua nyingine Mhe. Aweso amewasihi wananchi wa Ndelenyuma kulinda miundombinu ya miradi huo inayoletwa na kumpokea kwa kishindo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anaetarajia kuanza ziara mkoani Ruvuma wiki ijayi tarehe 23 Septemba 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *