NAIBU WAZIRI KIGAHE ATEKELEZA ILANI YA CHAMA KWA.KUJENGA BARABARA YA KIWANGO CHA LAMI VIJIJINI

0

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini anatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi Kwa asilimia 100,baada ya kufungua ujenzi wa barabara ya vijiji vya Ifwagi,Mtili na Mtupa yenye urefu wa kilomita 14.

Mara baada ya kukamilika Kwa barabara hiyo,atafungua ile Mdabula ihunwa yenye kiwango cha lami,ili kuzidi kuinua uchumi wa Mufindi Kaskazini.

Akizungumza akiwa eneo la ujenzi wa barabara unaoendelea kwenye vijiji hivyo,Kigahe amesema lengo lake ni kuona wananchi wa jimbo hilo wananufaika na ujenzi wa miundombinu unaofanywa katika maeneo hayo.

“Hapa tunatekeleza Ilani ya CCM inahitaji kuona wananchi wake kila kona wanafanya maendeleo kupitia uwekezaji unaofanywa na serikali,”alisema Kigahe.

Amesema Mufindi kuna wafanyabiashara wakunwa Kwa wadogo,hivyo wanahitaji kuona Miundombinu inaboreshwa kwa kiasi kikubwa ili waweze kusafirisha bidhaa zao.

Aidha amesema ujenzi wa barabara hiyo utakamilika na wananchi wataanza kuitumia kutoka sehemu moja kwenda nyingine ikiwemo kusafirisha mazao na bidhaa nyingine za biashara kwa urahisi.

Amesema wanajipanga kihakikisha wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini wananufaika na uje Zi wa barabara hiyo inayoendelea kujengwa katika vijiji hivyo.

Hata hivyo amewataka wakazi wa maeneo hayo,kiwa.na subira kwa sababu kazi inaenda vizuri na wakandarasi wako site kujenga miundombinu ya Barbara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *