MSANII WAKAZI – KIZAZI HIKI NI SENSITIVE KIASI HICHO, MAUAJI KIONGOZI WA CHADEMA
Sio kwenye filamu, sio kwa kushuhudia kwa macho… Nimeona jinsi nchi zingine ambavyo wanayapa maisha ya kila mtu kipaumbele!
Jeshi la Marekani wana kitu kinaitwa NO MAN LEFT BEHIND. Yaani hata ukichukuliwa mateka, au kuuwawa watakurudia.
Filamu ya “Saving Private Ryan” kikosi kizima kiliteketea, kisa kwenda kumuokoa mtu mmoja. That’s how others value LIFE, and LIVES OF THEIR PEOPLE. Israel ukimgusa mtu wao mmoja tu, anakushushia kipigo cha mwizi.
Tanzania kumekuwa na vitendo vya kihaini, tena ambavyo vinashukiwa kuhusisha vyombo vya dola, na hakuna actions wala kauli madhubuti za Viongozi wa juu za ku-prove their unequivocal stance! Zaidi kumekuwa na efforts za ku-undermine & spin politically.
Inasikitisha sana, na inaogopesha mno. Kwamba nchi ambayo inaitwa ya “Amani” na mji unaoitwa “Bandari ya Salama” (Dar Es Salaam), sasa hivi wananchi wake wanaanza kutembea na hofu, kweli? For fucking what?
Kizazi hiki ni sensitive kiasi hicho, kwamba mtu akiwa na opposing viewpoint, unamdhuru? Aren’t we a “multiparty democratic state” ?! Where are we heading?
Tupo tayari kufa kwaajili ya Taifa, ila sio kuuliwa nalo. Viongozi wakikaa kimya au kutochukua hatua nyakati kama hizi, ni sawa na ku-sign our death sentences.
Poleni CHADEMA, poleni Familia ya Marehemu! #Kibao🕊️🕊️