Mshambuliaji wa Marekani Alex Morgan ametangaza kustaafu soka katika mechi ya Jumapili timu yake ya San Diego Wave FC ilipotandikwa 4-1 nyumbani dhidi ya North Carolina kwenye ligikuu ya soka USA Morgan mwenye umri wa miaka 35 amefikia uamuzi huo wa kustaafu baada ya kujua kuwa ana ujauzito wa mtoto wake wa pili.

Mshindi huyo mara mbili mfululizo wa kombe la dunia 2015 na 2019 binti yake wa kwanza Charlie alizaliwa mwaka wa 2020, alikosa penalti dakika ya 10 ya mchezo wake wa mwisho na baadaye alitolewa sub na kutamatisha safari yake ya soka aliyoianza miaka16 iliyopita.

Morgan pia amewahi kushinda medali ya dhahabu akiwa na nchi yake kwenye Olimpiki ya London 2012.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *