DKT. TULIA AFUNGUA KITUO CHA AFYA CHAANI, ZANZIBAR

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mikoa ya Kaskazini na Kusini Unguja, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 27 Aprili, 2024 amezindua na kufungua Kituo cha Afya cha Chaani katika Jimbo la Chaani, Wilaya ya Kaskazini A kilichojengwa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Nadir Alwardy.

Wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Tulia pia ametoa msaada wa Shilingi Milion 10 kwa waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua hivi karibuni katika Mkoa wa Kaskazini, Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *