ASHTAKIWA KWA KUOMBA RUSHWA YA NGONO MKOANI TABORA

0

Aprili 25, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Tabora, mbele ya Mhe. Demetrio Nyakunga, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora, imefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi Namba ECC. 10892/ 2024 ya Jamhuri dhidi ya Bw. Michael Fredrick Mgongo  Mhadhiri katika Chuo Cha Utumishi wa Umma (TPSC) Tawi la Tabora. 

Mwendesha Mashtaka kutoka TAKUKURU Bi. Mwanaidi Mbuguni ameieleza Mahakama  kwamba mshtakiwa aliomba rushwa  ya ngono kwa mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (Uhazili) ili amfanyie upendeleo na kumfaulisha masomo aliyofeli.

Mshtakiwa alisomewa mashtaka yanayomkabili na kukana mashtaka hayo.

Mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na yuko nje kwa dhamana ambapo kesi hiyo itakuja tena 23.05.2024 kwa ajili ya kusoma hoja za awali kwa mshtakiwa na kuanza kusikilizwa kwa upande wa Jamhuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *