Timu ya Taifa ya Kandanda ya Tanzania (Taifa Stars), ambayo ilikuwa irejee nchini kesho tarehe 07 Januari, 2025, sasa itarejea tarehe tarehe 08 Januari, 2026.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, amesema mabadiliko hayo yana lengo la kuiwezesha timu hiyo kuwasili muda mzuri ambao utatoa nafasi kwa Watanzania kuwapokea na kuwapongeza wachezaji kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya wakiwa katika mashindano makubwa ya kandanda Barani Afrika (AFCON2025) yanayofanyika nchini Morocco.
Kulingana na mabadiliko hayo sasa Taifa stars itawasili nchini keshokutwa tarehe 08 Januari, 2026 majira ya saa 4:00 asubuhi na kupokelewa na wananchi wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.
Msigwa ametoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam kujitokeza kuwashangilia na kuwapongeza mashujaa wetu Taifa Stars kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya nchini Morocco.