Leo Januari 7, 2026. Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole Mh. Dkt.Tulia Ackson ametembelea kata ya Igawilo kujionea daraja lililovunjia mtaa wa Mponja.
Daraja hilo lilikuwa likitumika na wananchi wa kata hiyo kutoka mtaa mmoja kwenda mtaa mwingine ambapo chanzo cha daraja hilo kuvunjika ni kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha ambapo Dr. Tulia ameahidi kutatua changamoto hiyo haraka.
Mbali na hilo Dkt. Tulia amewasihi wananchi waache kutupa taka kwenye mifereji ya maji kwani hali hiyo inasababisha kufanya mifereji kuziba na kusababisha athari mbaya kwa jamii kwa ujumla.
Amemalizia kwa kusema, “Viongozi acheni kuwauzia watu maeneo ambayo yanachangamoto ya maji kujaa ili kuepukana na adha ya mafuriko pindi yatakapotokea” ameongea hayo kutokana na baadhi ya maeneo kuwa na changamoto ya kupata mafuriko sababu ni watu kujenga katika maeneo hatarishi yanayopelekea kuzuia mkondo wa maji kwenda inavyotakiwa na kupelekea Mafuriko.



