TUSITUKANANE WALA KUBAGUANA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA- NAIBU WAZIRI MKUU DKT. BITEKO
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko amesisitiza kuwa Bonanza la Bunge liwe chachu ya kuwakumbusha Umuhimu wa kuchagua Viongozi walio Bora katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bila kuruhusu kubaguana na kutukaniana
Amesisitiza hayo Leo 31 Agosti, 2024 katika Viwanja vya Shule ya John Merlin Jijini Dodoma wakati wa Bonanza la Bunge Kwa Udhamini wa NMB.
“Bonanza hili liwe chachu ya kutukumbusha Umuhimu wa kuchagua Viongozi wanaofaa, watakaotuunganisha Watanzania bila kujali makabila Wala vyama, Kiongozi wa Kitongoji au Mwenyekiti wa Kitongoji au Kijiji tusiwachukulie poa wakati wa Uchaguzi huu”
Aidha NMB Kwa kutambua umuhimu Kwa Jamii wamekabidhi Hundi ya Kiasi Cha Tsh Milioni 50 kwaajili ya Shule ya Sekondari ya wavulana ya Bunge.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa IPU Mhe. Dkt. Tulia Ackson amewashukuru Benki ya NMB Kwa kutoa kiasi cha Tsh Milioni 50 kama mchango wao kuunga mkono juhudi za Bunge kwaajili ya Kujenga Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Bunge.
Ametoa Wito Kwa wadau kuendelea kutoa michango kwaajili ya Kujenga Shule hiyo ambayo itakuwa ni Bora
Wadhamini wa Bonanza hilo Benki ya NMB kupitia Kwa Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu NMB-Juma Kimori amesema Wana program ya kuhakikisha wanafika kila Kijiji nchini kupeleka Huduma na hivyo kuwaomba wabunge kuwapa ushirikiano Kwa kuwa Mabalozi wazuri kwenye maeneo yao.
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club-Mhe. Festo Sanga (Mb) amesema Bonanza hilo ni sehemu ya maandalizi kuelekea mashindano ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA)
Bonanza hilo lililoanza Kwa Matembezi Mapema Saa 12 Asubuhi kutokea Chuo Cha Mipango hadi Viwanja hivyo vya Shule ya John Merlin imeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Pete, Mpira wa Miguu, Kuvuta Kamba, Kukimbiza Kuku, kuvaa Soksi, Kula chakula na kunywa soda, Mchezo wa rede, Pull Table na mingine mingi