UWEZO YATOA MAFUNZO YA STADI ZA UFUNDISHAJI LUDEWA
Walimu zaidi ya 40 kutoka katika shule 20 Wilayani Ludewa Mkoani Njombe, wameanza mafunzo ya mbinu za stadi za kufundisha Ili kukuza kiwango Cha ukuaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).
Mafunzo hayo ambayo hutolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Uwezo yamezinduliwa rasmi na Afisa Elimu msingi Mkoa wa Njombe Nelasi Mulungu kwa niaba ya Katibu Tawala mkoa Bi. Judica Omary.
Bi. Malungu amesema kuwa tatizo la KKK kwa mkoa wa Njombe lipo hasa kwa wanafunzi wa darasa la kwanza, lapili na darasa la tatu hivyo mafunzo hayo yatakuwa chachu ya ukuaji wa elimu kwa wanafunzi hao.
Grayson Mgoyi ni Mkuu wa Idara ya mawasiliano na uchechemuzi kutoka shirika la Uwezo Tanzania amesema mafunzo haya kwa Wilaya hiyo ya Ludewa yanafanyika kwa mara ya pili ambapo mwaka uliopita walimu 80 kutoka katika shule 40 walipatiwa mafunzo hivyo na sasa insfikisha jumla ya walimu 120 waliopata mafunzo Wilayani humo.