SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA HALI YA HEWA

0

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuendelea na jitihada za kukuza uchumi wa Nchi zinazoenda sambamba na uboreshwaji wa miundombinu na huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo hali ya hewa.

Akizungumza leo Agosti 21, 2024 jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari yenye lengo la kujadili namna bora ya kufikisha taarifa kwa wananchi kuhusu utabiri wa mvua za msimu wa Vuli unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba hadi Disemba 2024.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Mabadiliko ya Sayansi ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema kuwa serikali itaendelea kufanya uwekezaji katika miundombinu ya hali ya hewa kupitia mpango wa bajeti na program mbalimbali za maendeleo.

Dkt.Chang’a amesema kuwa TMA imeendelea kutoa huduma za utabiri wa hali ya hewa maeneo madogo kwa wilaya zote mikoa iliyopo katika ukanda unaopata mvua za vuli ili kuhakikisha inawasaidia wakulima, wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuweza kuchukua tahadhari kwa lengo la kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

“Katika mkutano huu wanahabari mtaendelea kupata uelewa kuhusu sayansi ya hali ya hewa kupitia rasimu ya utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2024, hivyo ni muhimu kufatilia kwa ukaribu kuona namna bora ya kuwahusisha wadau katika sekta zao ili kukabiliana na hali ya hewa inayotarajiwa kwa kutambua kuwa ninyi ni daraja baina yetu na watumiaji wa taarifa zetu” amesema Dkt.Chang’a.

Amesema kuwa lengo kufikisha taarifa sahihi za hali ya hewa pamoja na athari zake kutokana zina umuhimu mkubwa ikiwemo kupanga utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii.

Mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli 2024 unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba hadi Disemba 2024 ambapo umebeba kauli mbiu isemayo : Matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kwa wote na wakati.

Imeandaliwa na Noel Rukanuga – DSM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *