UPATIKANAJI WA MAJI ARUSHA NI KWA SAA 21″- MHANDISI RUJOMBA

0

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha Mhandisi Justine Rujomba amesema Maji katika jiji la Arusha kwasasa yanapatikana kwa saa 21 kwa siku na lengo ni kuhakikisha upatikanaji wake unakuwa kwa saa 24.

Mhandisi Rujomba ameyasema hayo leo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, kwenye kikao alichokiitisha Mhe. Makonda ili kujadili juu ya upatikanaji wa maji kwenye Mkoa wa Arusha na namna ya kudhibiti visababishi vinavyosababisha changamoto za upatikanaji wa maji safi.

Aidha Mhandisi Rujomba amekiri uwepo wa athari kubwa ya mabadiliko ya tabianchi kwenye upatikanaji wa maji, akisema chemchem nyingi zimepunguza uzalishaji wa maji ya kutosha suala ambalo limeifanya serikali kuanza kuchimba visima ili kusaidia kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *