RAIS SAMIA MGENI RASMI MAONESHO YA KILIMO YA KIMATAIFA NANE NANE 2024

0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, leo Agosti 07, 2024 ameongoza zoezi la ugawaji wa zana za kilimo za kisasa kwa wakulima 12. Zoezi hilo limefanyika kwenye Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma ikiwa ni kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Nanenane Kimataifa Agosti 08, 2024.

Zana hizo za kilimo ambazo zimegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 845, zimetolewa na Kampuni ya PASS learning inayojihusisha na udhamini kwa wakulima wasio na uwezo wa kununua zana bora na za kisasa za kilimo kupata zana hizo kwa mkopo nafuu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Mkoa huyo amesema; “Napongeza zoezi hili kwani linatufanya kuja kushuhudia Mapinduzi makubwa ya Kilimo hapo mbele na hii inadhihirisha kuwa Wakulima sasa wanafahamu umuhimu wa kutumia zana bora za kilimo”

Kampuni ya PASS learning imedhamini ugawaji wa matrekta ya Kilimo 12, gari 1 kubwa la kubebeba bidhaa za kilimo na mashine 1 yenye uwezo wa kuchakata aina tisa za mazao. Zana hizo nitakwenda kuwanufaisha wakulima takribani 700 wa Mikoa ya Kanda ya Kati ikiwemo Dodoma, Morogoro, Singida na Morogoro.

Wakati huo huo, Mhe. Senyamule, ametumia jukwaa hilo kutoa taarifa kwa Umma juu ya kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Nanenane Kimataifa zinazofanyika kwenye Mkoa wa Dodoma kuwa yatahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja hivyo siku ya Alhamisi Agosti 08, 2024 kushuhudia namna teknolojia mbalimbali zinazoweka kutumia kwenye kilimo, Mifugo na Uvuvi zinavyoweza kusaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *