SILINDE AITAKA TFC KUHAKIKISHA WAKULIMA WANAPATA MBOLEA YA RUZUKU KWA WAKATI

0

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde ameielekeza Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kuhakikisha wakulima wote nchini wanapata mbolea ya ruzuku kwa wakati ili kuwasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ili kufikia azma ya Serikali kuhakikisha Sekta ya Kilimo inakuwa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030 na kuongeza kipato kwa wakulima.

Mhe. Silinde ametoa maelekezo hayo katika Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayoendelea katika Kanda mbalimbali nchini huku Kitaifa yakifanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma alipofika kwenye banda la Kampuni hiyo kwa nyakati tofauti kufahamu namna ilivyojipanga na msimu mpya wa kilimo.

Vilevile, Silinde amehimiza kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wakulima wanapata huduma kwa wakati kwani Serikali imewezesha fedha nyingi illi kuhakikisha wakulima wanapata huduma hiyo.

Akitoa ufafanuzi namna TFC ilivyojipanga, Afisa Masoko wa Kampubi ya Mbolea Tanzania Bw. Laurent Otaru ameeleza kuwa mojawapo ya mikakati iliyoweka na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) ni kuongeza idadi ya mawakala wapya watakosaidia kusambaza mbolea kwa urahisi na pia kushirikiana na Vyama vya Ushirika ili kuwafikia wakulima wengi zaidi hususani maeneo ya Vijijini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *