WANAUME HAKIKISHENI MNASAPOTI VIPAJI VYA WANAWAKE ZENU.

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekuwa chachu ya maendeleo Kwa wanawake Kwa kuwapigania na kuinua Vipaji vyao.

Uthibitisho huo umetolewa na Mshereheshaji wa Like nchini Tanzania kutokea Dodoma Devota Felix Maarufu Mc Devoti wakati akizungumza na Wanahabari katika Hafla yake aliyoiandaa kwaajili ya kula chakula Cha Jioni na Jamii yake ikiwemo wanaomsapoti kwenye Kazi zake.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuishukuru Jamii Kwa namna ambavyo imekuwa ikimuunga mkono katika Kazi zake hadi kufikia kunyakua Tuzo mbalimbali ikiwemo Dina Marious na Mwanamke Mwamba.

“Mama Samia Suluhu Hassan hatumwangalii tu kama Kiongozi bali tunamwangalia kama mwanamke ambaye ni Mama na anaweza kuishika Nchi vizuri na maendeleo yakapatikana na sisi tunapata Ari na Moyo wa kuendelea kufanya Vizuri hususani kurudisha kwenye Jamii”

Mwanamke huyo Mwamba ambaye ni mwajiriwa wa Serikalini lakini Bado anapambana katika shughuli za Ushereheshaji ametoa Wito kwa Wanaume kusapoti Vipaji vya wanawake zao na kuamini katika vipawa walivyonavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *