ZAIDI YA WASANII 20 WALAMBA DILI NONO LA UBALOZI WA MATI SUPER BRANDS LTD
Head quarters za kampuni ya Mati Super Brands Ltd mjini Babati Mkoani Manyara zimetembelewa na wasanii zaidi ya 20 wa muziki wa Bongo flava Old School na New school wakiongozwa na muandaaji mkongwe wa muziki P.Funk Majani @majani187 .
Wasanii hao wameshuhudia utiaji saini wa ubalozi na ushirikiano wa kibiashara katika nyanja mbalimbali kati ya kampuni ya Mati Super Brands Ltd pamoja na lebo ya Muziki ya Bongo Records, ambapo wasanii hao wamelamba dili nono la ubalozi wa baadhi ya bidhaa za Mati Super Brands Ltd zikiwemo Tanzanite Royal Gin, Tanzanite Premium Vodka na Strong Dry Gin.
Huu ni muendelezo wa mapinduzi ya kibiashara na matangazo kwa kampuni ya Mati Super Brands Ltd hasa kupitia sekta ya Burudani na Michezo baada ya hivi karibuni kuingia mkataba wa udhamini na klabu ya mpira wa miguu ya Fountain Gate.
Mkurugenzi wa Mati Super Brands Ltd David Mulokozi amesema kuwa licha ya kutumia wasanii hao kutangaza bidhaa za kampuni lakini lengo pia ni kuendelea kukuza muziki wa Tanzania kwa kuwawezesha wasanii kiuchumi kupitiaa mikataba ya ubalozi.
Miongoni mwa wasanii waliofika katika tukio hilo ni pamoja na Juma Nature, Rapcha, Q chilla, Mr Blue, Stamina, Jay Mo, Lina, TID, Mandojo na Domokaya, Inspector Haroun, Dipper Rato, Ferouz, Afande Sele, Matonya na wengine wengi.