MTOTO WA MIEZI MIWILI ANYONGWA NA MAMA YAKE MPAKA KUFA KWA KUTUMIA KIPANDE CHA KITENGE.

0

Jeshi la polisi mkoa wa Geita linamshikilia Frola Malopu mkazi wa kijiji cha mienzi wilayani Bukombe kwa tuhuma za kumnyonga mtoto wake wa miezi miwili mpaka kufa kwa kutumia kipande cha nguo aliyokuwa amaevaa baada ya kuugua akiwa njiani kipindi anaenda kwa mume wake akisema atamsumbua huko aendako.

Ameyabainisha hayo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwakwe ambapo alisema mama huyu alijifungua watoto wapacha wakike na wakiume ambao walikuwa wa mwanaume mwingine tofauti na Yule mme wake wa mwanzo baada ya kukosana na baba wa watoto hao aliamua kurudi kwa mme wake wa mwanzo akiwa njia motto wa kike alianza kulia ndio akaamua kumnyonga ili asiendelee kumusumbua.

Baada ya mwili wa mtoto huyo kupatikana alikutwa akiwa amenyofolewa baadhi ya viungo vyake mama wa mtoto alipoulizwa alikiri kumuua mtoto huyo lakini kuhusu kuondolewa kwa viungo vyake alikana kuhusika hivyo jeshi la polisi linaendelea kuwasaka wale wote waliohusika katika tukio hilo.

Katika tukio lingine jeshi la polisi linawasaka mme na mke kwa tuhuma za kumkata viganja ya mikono Rehema Paulo (26) mkazi wa katente wilayani Bukombe huku chanzo cha tukio hilo likiwa ni wivu wa kimapenzi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *