NBC DODOMA MARATHON 2024 KUSAIDIA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, amefanya Mkutano na waadishi wa habari kwenye ofisi yake iliyopo jengo la Mkapa Jijini Dodoma kuutangazia umma kuhusu mbio za NBC Marathon zinazotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili, tarehe 28 Julai 2024.

Katika Mkutano huo, Mhe. Senyamule amebainisha lengo la mbio hizo ambazo zinatarajia kushirikisha takribani watu elfu kumi na mbili watakaoingia katika Mkoa wa Dodoma.

“Lengo kuu la mbio hizi ni kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya Saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake nchini pamoja na ufadhili wa masomo kwa wakunga kwa kupitia taasisi ya Bebjamini Mkapa. Saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoongoza kwa kuchangia vifo zaidi vya wanawake.” Rc Senyamule

Aidha, amesema kuwa mbio hizo zitaleta fursa za kiuchumi katika mkoa wa Dodoma kwani idadi hiyo ya watu itahitaji malazi, chakula, mavazi, vinywaji na usafiri hivyo, ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo.

“Nichukue fursa hii kuwashawishi wananchi wa Dodoma kuchangamkia fursa hii kwa kuweka biashara zao tayari na kuhakikisha wanatoa huduma stahiki na hivyo kujiongezea vipato vyao. Wageni wetu watahitaji huduma zote za kijami na sisi kama wenyeji ni lazima tujipange vilivyo” Ameongeza Mhe. Senyamule.

Mbio za NBC Dodoma Marathon zinafanyika kwa mara ya tano mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri kwa ushirikiano na Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na zinatarajiwa kuwa hadi Km 21.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *