SILINDE AWAHAKIKISHIA WAKULIMA UJENZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI ZA SOKO NA BWAWA LA URENGA WILAYANI MOSHI

0

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amesema Serikali imepanga kufanya usanifu wa kina ili kupata gharama halisi za ujenzi wa miradi ya umwagiliaji ya Skimu ya Soko yenye ukubwa wa hetka 38,000 iliyopo kata ya Kahe Magharibi, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro pamoja na ujenzi wa Bwawa la Urennga katika kijiji cha Meru kata ya Kirua Vunjo Mashariki, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri Silinde ameyasema hayo tarehe 24 Julai 2024 alipotembelea miradi hiyo na kuwaeleza wananchi kuwa Wizara ya Kilimo itawatuma Wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa ajili usanifu wa kina ili miradi hiyo iwekwe kwenye mpango wa bajeti kwa ajili ya ujenzi.

Awali akitoa taarifa za skimu ya Soko, Mhandisi Fridolin Mpanda, Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Moshi amesema kuwa wakulima katika skimu ya Soko wamekuwa wakilima kwa makundi kila awamu kutokana na upungufu wa maji na kukosena kwa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu hiyo.

Aidha, Mhe. Silinde amesema Serikali itaendelea kuboresha skimu zote za zamani pamoja na kujenga skimu mpya za umwagiliaji. Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutawawezesha wakulima wa skimu hizo kuzalisha katika misimu yote ya mwaka bila kutegemea mvua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *