WAZIRI KAIRUKI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA PILI WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI KUHUSU UTANGAZAJI UTALII- KANDA YA AFRIKA NCHINI ZAMBIA

0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Pili wa Shirika la Utalii Duniani – Kanda ya Afrika (Brand Africa ) Kuhusu Utangazaji Utalii unaoongozwa na mada isemayo: “Kuitangaza Afrika kwa lengo la kufungua fursa za Uwekezaji na Maendeleo ya Sekta ya Utalii”.

Pamoja na mambo mengine mkutano huo umejadili masuala ya kukuza utangazaji utalii na taswira ya Bara la Afika kwa kuandaa maudhui yanayoliuza Bara hilo lengo ikiwa ni kuvutia watalii wengi zaidi.

Mkutano huo unafanyika leo Julai 23, 2024 katika hoteli ya Avani Victoria Falls Resort, jijini Livingstone Zambia ukihusisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kutoka nchi wanachama wa Shirika la Utalii Duniani.

Mhe. Kairuki ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Ephraim Mafuru, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Richie Wandwi pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bodi ya Utalii Tanzania.

Pia, Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Usafirishaji Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo na Mkurugenzi wa Bodi ya TATO, Vesna Tibaijuka wameshiriki mkutano huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *