RAIS SAMIA KUMNUNULIA MGUU WA BANDIA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA MGUU

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo asimamie shughuli zote za matibabu ya mtoto mwenye ulemavu wa mguu aliyejitokeza katika mkutano wa njiani wakati akiwasalimia Wananchi wa Tunduma akielekea Dodoma Mara baada ya Kumaliza Ziara yake Mkoani Rukwa leo tarehe 18 Julai, 2024.

Mhe.Rais amesema gharama zote za matibabu kumhusu mtoto huyo zitakua chini ya ofisi yake na kama kutakua na hoja yakuletwa Dar es salaam basi apelekwe haraka kwaajili ya hayo matibabu

Rais wa Tanzania Dkt. Samia ametoa maagizo kwa Ofisi yake pamoja na Wizara ya Afya kuhakikisha Mtoto Ebenezer Wile Mwaksyle (8) ambaye ni mlemavu aliyekua pembezoni mwa Barabara alipokua akihutubia Wananchi wa Tunduma atengenezewe mguu wa bandia mara moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *