HAIWEZEKANI KILA KIONGOZI ASHUGHULIKIE MATATIZO YA ARDHI

0

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amesema migogoro ya ardhi bado ni changamoto kubwa hapa nchini ambayo imeathili viongozi na wananchi licha ya serikali kuendelea kupambana kulitatua tatizo hilo.

Simbachawene ameyasema hayo leo Jun 19 wakati akizindua maonyeshoya ya wiki ya utumishi wa umma yanayoendelea jijini Dodoma na kutalajiwa kutamatika June 23 ambapo amewataka viongozi wa serikali kuungana na kutatua migogoro ya ardhi nchini kwa pamoja.

“Sioni kama ni afya pale unapokuta karibu watu wote tunafanya kazi ya sekta moja sasa hii sekta Nathaniel kuna haja ya viongozi wote kuungana na kushirikiana kufanya kazi kwa pamoja katika kuhakikisha hawa wote wanaovunja sherianza za nchi wanashughulikiwa ote wanaofoji nyaraka za serikali polisib wakamateni muwafungulie kesi za jinai” Amesema Waziri Simbachawene.

Aidha Waziri Simbachawene amesema moja kati ya sababu ya ya sekta hiyo kuwa na migogoro mingi ni pamoja na baadhi ya watumishi kushindwa kutimiza wajibu wao pamoja na upungufu wa watumishi kwenye sekta ya ardhi.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Riziwani Kikwete amezielekeza wizara na taasisi zake kuendelea kutumia mifumo ya tehama ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

DKT Khamis Amani ni Makamu mkuu wa chuo cha utumishi wa umma ambaye amesema chuo chao kimeendelea kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo na sababu za kwa nini baadhi ya watumishinwamekuwa wakitumia vibaya Madaraka na Mali za umma kitu ambachokimepelekea kuanza kutia mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajengea uwezo wa tumishi ilibwaweze kuzingatia maadili ya utawala Bora.

“Sasa hivi tuna mpango wa mafunzo ambao umeanzishwa kwa watumishi wa umma kulikuwa na tatizo la kukosekana kwa mafunzo hayo lakini hivi sasa tumehakikisha mafunzo hayo yanatolewa mara kwa mara kwa watumishi wote ili kiwajengea kuufahamu maadili nanmisingi ya utumishi wa umma” amesema Dkt Khamis Amani.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu ofisi ya idara ya kumbukumbu Firimini Mssiangi
Amewataka watanzania kuendelea kujitokeza kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu nyarajaka za serikali na viongozi mbalimbali wa serikali waliopita kama maraisi wa awamu zilizopita huku akiahidi kuendelea kuzitunzq vyema nyaraka za serikali kwa ajili ya matumizi yankizazi kijacho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *