SPIKA DKT. TULIA ATOA MSAADA KWA BINTI MWAJUMA MASENGO – RUVUMA

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 14 Juni, 2024 ametoa msaada wa kiti mwendo kwa Binti Mwajuma Masengo (22), mkazi wa Kata ya Lituta Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma ambaye ni mlemavu wa viungo.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amemsaidia Mama mzazi wa Binti huyo Bi. Teodosia Kibumo, kiasi cha Shilingi Milioni moja kwa ajili ya kumuwezesha kukuza biashara yake wakati akiendelea kumtunza binti yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *