ASKARI MSIWE NA HURUMA NA WANAOKIUKA SHERIA ZA BARABARANI, NI WAUAJI.
“Takwimu zetu za ajali zitokanazo na vyombo vya moto zinaashiria hatari kubwa sana ambayo kila mtu anapaswa kuongeza umakini, Watanzania wengi bado hatuheshimu sheria za barabarani, hatuna nidhamu na matumizi ya vyombo vya moto na alama za barabarani,
Madhara yake tunapoteza nguvu kazi ya nchi yetu kutokana na ajali za barabarani ambazo zinatuondolea watu wanaotegemewa katika jamii zetu, “
“Wakati mwingine kwa uzembe unaoweza kuepukika, Katika kipindi cha miaka mitano yaani kutokea mwaka 2019 hadi Mei 2024, ajali za barabarani zilikuwa 10,093 ambapo vifo vilikuwa 7,639 na majeruhi 12,663 miongoni mwao wakipata ulemavu wa kudumu,”
Akiwasilisha Mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25 Leo Alhamisi Juni 13,2024 Bungeni Jijini Dodoma Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema “Hebu fikiria, magari binafsi – ajali 3,250, vifo
2,090, majeruhi 3,177. Hebu fikiria, mabasi – ajali 790, vifo 782, majeruhi 2,508. Hebu fikiria, daladala – ajali 820, vifo 777, majeruhi 1,810. Hebu fikiria, taxi – ajali 93, vifo 97, majeruhi 173. Hebu fikiria, magari ya kukodi (sherehe,
misiba, na shughuli maalum) – ajali 326, vifo 263, majeruhi 302, Idadi hii kubwa ya majeruhi na vifo vya watu kutokana
na ajali utadhani nchi iko kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, Jambo Hili Halikubaliki!,”
“Mheshimiwa Spika, ilivyo sasa wengi huona usumbufu na wakati mwingine mpaka tunaweka chuki na uadui tunapokumbushwa kuhusu usalama wetu na Jeshi la Polisi tuwapo barabarani, Tunavunja sana sheria barabarani, hata magari ya Serikali hivyo hivyo, wakati mwingine
tunawagonga waenda kwa miguu, Ni wakati sasa jambo hili kuazimiwa na jamii nzima ya watanzania kwa kuweka mtazamo wa kuchukia ajali,”
“Mheshimiwa Spika, kama sheria zetu ni rafiki sana, tuyaondoe makosa yote ya ajali barabarani kwenye inayoitwa traffic case, tupeleke kwenye makosa makubwa zaidi
ikiwezekana huu uwe ni uuaji kama uuaji mwingine kwa maana mtu anayekufyatulia risasi kwa kukusudia ana uhakika kuwa atakujeruhi au kukuua na hata anayefanya
uzembe na vyombo vya moto ana uhakika wa kukujeruhi au kuua kwa makusudi kabisa,”