MBUNGE FATMA TOUFIQ AGAWA MITUNGI 200 YA GESI KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MPWAPWA
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Dodoma Mhe Fatma Toufiq amemuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhimiza Nishati safi ya kupikia ikiwa ni agenda ya kumtua Mama kuni kichwani.
Hiyo ni miongoni mwa mkakati jumuishi wa kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili mpaka kufikia 2034 wananchi zaidi ya 80% wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi na mkaa ulioboreshwa.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 200 kwa wanawake wajasiriamali,mama lishe wa Wilaya ya Mpwapwa Iliyotolewa kwa Ushirikiano wa Kampuni ya Oryx iliyofanyika jana tarehe 4 june 2024, Mbunge toufiq amewataka wanawake hao kutumia nishati ya gesi katika shughuli zao za ujasiriamali na kuepuka matumizi ya kuni.
“ule utaratibu wa kukimbizana na mikaa,kuni lakini sasa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan anataka kumtua Mwanamke kuni kichwani badala yake aweze kutumia nishati safi na salama”
Aidha, ameahidi kuendelea na programu hiyo kwa wakinamama wa wilaya zote za Dodoma ili kuwatua kuni kichwani na kusaidia kulinda mazingira.