MSITUMIE DAWA KIHOLELA – WAZIRI UMMY MWALIMU
Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu ameitaka jamii kuacha matumizi ya dawa za Kutibu maambukizi ya bacteria (Antibaotiki) kiholela jambo ambalo linapeleka usugu wa vimelea vya magonjwa.
Waziri ummy ameyasema hayo katika mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa jamii kuhusu kuimarisha huduma za afya ngazi ya msingi kwa ushirikiano wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Odo Ummy Foundation pamoja na Taasisi ya Apotheker ili kuwajengea uelewa wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazo ikabili jamii hususani ni katika sekta ya afya.
“Sasa hivi kuna matumizi yasiyo sahihi ya dawa za antibiotiki mtoto ameumwa tumbo kidogo la kuharisha mzazi unaenda duka la dawa unanunua dawa za antibiotik matokeo yake tumesababisha usugu wa vimelea vya magonjwa hali inayo pelekea kila dawa za anti kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Mtoto akiharisha apewe ORS – Zink. Antiobiotik ni hadi aandikiwe na Daktari. Alisema Waziri Ummy.
“Kwa sasa matumizi ya dawa za antibiotik yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 65% na Shirika la Afya Duniani (WHO) lina sema kwa wagonjwa wanao lazwa tusifike asilimia 30% sasa tupo asilimia 65%”
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Sera wa Apotheker, Dr Suleiman Kimatta alisema kuwa magonjwa mengi kama vile ukimwi,kifua kikuu,malaria kuna vimelea vinavyo sababisha magonjwa hayo hivyo ni muhimu kumeza dawa sahihi ili kuweza kuua vimelea kwani ukitumia dawa kiholela inapelekea kimelea kuwa sugu na kuhatarisha afya yako pamoja na kifo.