ALBINO ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUKATWA MAPANGA GEITA
Mototo mmoja mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) Kazungu Julius, mwenye umri wa miaka 10 mkazi wa katoro mkoani Geita amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kisa kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi ambapo amelazwa katika hospitali ya halmashauri ya mji Geita.
Akisimulia tukio lilivyotokea mama mzazi wa mtoto huyo Frola Nzumbe amesema mtoto wake alivamiwa na mtu asiyejulikana akiwa na mapanga wakati mtoto wake akitoka kuoga ambapo alimkata maeneo mbalimbali ndipo akapiga kelele kuomba msaada kwa majirani ili waweze kumpeleka hospitali kutoka na hali yake kuwa mbaya kwa kutoka damu nyingi sana.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mji Geita Dokta Thomas Mafuru amesema walimpokea mtoto huyo akiwa katika hali mbaya usiku saa 5 siku ya jumatano ndipo alianza kumpatia matibabu kwa kumshona katika majeraha yake na anaendelea vizuri kwasasa.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi SACP Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hiyo na kusema wanaendelea na uchunguzi kubaini wahusika wa tukio hilo ili waweze kuchukuliwa hatua huku akiwatoa hofu watu wenye ulemavu wa ngozi mkoani Geita kuwa atahakikisha anaimarisha usalama wao.