“ACHANENI NA MATENDO YANAYOKIUKA MAADILI” MBUNGE TOUFIQ

0

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Fatma Toufiq amesisitiza umuhimu wa Elimu kwa Viongozi wa Bakwata waliofuzu Mafunzo ya Bakwata Online Academy pamoja na kuendelea kupinga, kukemea na kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia pia amewataka kuwa na maadili mema, kufuata sheria na taratibu za nchi na kuachana na matendo yote yanayokiuka maadili

Amesisitiza hayo wakati ameshiriki hafla ya mahafali ya awamu ya saba kitaifa chini ya BAKWATA ONLINE ACADEMY (BOA) yaliyofanyika katika Viwanja vya Masjid Gadaf Jijini Dodoma.ambapo Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mhe.Dkt.Abubakar Zubeir Ally na Mgeni maalumu katika hafla hiyo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.

Mahafali hayo yameongozwa na Kauli mbiu “Elimika Badilika”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *