MABALOZI WAOMBWA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII
Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kwa kushirikiana na Benki ya Azania wamewaomba mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kutangaza vivutio vya utalii sambamba na kuwapa uhakika wa huduma bora za kifedha hapa nchini wawekezaji wanaokuja nchini.
Ombi hilo liliwasilishwa kwa mabalozi kufuatia kikao kazi kwa njia ya mtandao kilichofanywa kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na mabalozi hao kisha kufuatiwa na hafla maalum ya uwekezaji.
Hafla hiyo ya “Usiku wa Uwekezaji” ililenga kuwaonesha fursa za uwekezaji zilizopo nchini ikiwemo fursa zinazoendana na matukio wakati huu ambapo Tanzania kwa kushirikiana na Kenya na Uganda zinatarajiwa kuwa wenyeji wa michuano ya AFCON2027.
Mbali ya fursa za uwekezaji pia mabalozi hao wameelezwa fursa za kifedha ambazo wawekezaji wanaweza kunufaika nazo kupitia benki ya Azania ambayo inamilikiwa kwa ubia wa taasisi za mifuko ya hifadhi za jamii na wawekezaji binafsi.
Warsha ya Mabalozi inayofanyika kwenye Chuo cha Uongozi cha Mwl. Nyerere, Kibaha mkoani Pwani.