BASHUNGWA ASHIRIKI MAOMBI NA DUA YA KULIOMBEA TAIFA

0

Waziri wa wa Ujenzi Innocent Bashungwa, ameungana na Watanzania kushiriki Siku ya Maombi na Dua ya kuliombea Taifa katika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Tarehe 22, Aprili 2024.

Maombi hayo yanafanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ambapo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.

Kauli mbiu: “Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *