“MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU KITAIFA KUFANYIKA JIJINI TANGA” WAZIRI PROF. MKENDA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 yatafanyika jijini Tanga kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 31 mwezi Mei 2024 katika viwanja Vya Shule ya Sekondari ya Popatlal na mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ambaye atazindua Maonesho hayo na Mgeni rasmi katika kilele Cha Maadhimisho hayo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Prof.Mkenda ameyasema hayo leo April 09,2024 alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Ofisini kwake Jijini Dodoma
.
Waziri Mkenda amesema katika Kipindi cha mwaka 2019 hadi 2023, zaidi ya Bunifu 2000 zimetambuliwa na bunifu 283 kati ya hizo zinaendelezwa, na pia amesema bunifu 42 zimeweza kufikia hatua ya kubiashalishwa na zipo sokoni.
“Bunifu hizo zinatumika kutatua Changamoto Mbalimbali katika sekta za Kilimo,Maji,Nishati,Afya,na Elimu” alisema Mkenda.
.
Mkenda amesema Maadhimisho hayo kwa mwaka 2024 yatahusisha mambo yafuatayo; Maonesho ya Bidhaa,Bunifu na Teknolojia Mbalimbali, Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU), Mashindano ya Ujuzi (Skills Competition) kwa wanafundisha wa Vyuo Vya Ufundi na UfundiStadi hapa nchini, Kutakuwa na Mikutano na Midahalo Kuhusu Elimu, Ujuzi, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na Kutakuwa na Mafunzo kwa Wabunifu.
.
Aidha,Mkenda amesema Mwaka Huu wanatarajia kuwa na washiriki kutoka taasisi za Umma na Binafsi zipatazo 339 watakaojumuisha Vyuo Vya Elimu ya juu,na taasisi Mbalimbali kutoka Nje na Ndani ya nchi watashiriki.
.
Kwa upande mwingine, Waziri Mkenda amezialika Taasisi za Umma na Binafsi,Mashirika,Wizara na Wadau wengine wa ndani na nje ya Nchi kuendelea kujiandikisha kushiriki katika Maadhimisho hayo.