SAGINI ATAKA VIJANA WAFUNDISHWE MAADILI MEMA NA KUJIEPUSHA NA MAMBO YA HOVYO

0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb) amesema kuwa, ni vema Vijana wakajengwa na kujikita kwenye misingi ya maadili mema balada ya kujiingiza kwenye mambo yaliyo kinyume na mila na desturi zetu.

Akizungumza Machi 23, 2024 wakati wa Mashindano ya Fani za Usomaji wa Qur’aan yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa NSSF Ilala Jijini Dar es Salaam, alisema kuwa, maeneo mengi vijana hawaitilii elimu mkazo lakini ikija kwenye majukwaa ya unenguaji kwasababu watu wanawazawadia sana sasa uelekeo wa vijana wote ni huko ingawa bado kuna nafasi kubwa ya kuwafundisha na wakaondoka taratibu kwenye mambo yasiyofaa na hapa nisisitize kuwa sisi kama wasaidizi wa Mhe. Rais hatuwezi kufumbia macho vitendo hivyo tutapigana kufa na kupona ili vijana wetu wawe salama.

Aidha, Mhe. Sagini alisema kuwa kila elimu yenye manufaa kwa mwanadamu ni elimu inayofaa kwa kila mtu awe muislamu au mwingine uamuzi wa kuandaa vijana wakaingia sehemu zote unazaa matunda, kwani Baba wa Taifa alisema kuwa “Tunapowaelimisha vijana tukawatoa nje ya maeneo yetu kwenda mbali kusoma ni kama vile kijiji chenye njaa kinawatoa vijana kwenda safari za mbali kwenye jamii nyingine kutafuta chakula”

“Hao watu wakienda kule wakakitafuta hicho chakula wakakipata matarajio ni kwamba walete chakula kwenye jamii iliyowatuma, wakienda wakabaki huko wasirudi wakati huku watu walijinyima wakawapa wao fedha ili waende mbali watu hao huwa wasaliti na hawafai kwenye jamii” alisema Mhe. Sagini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *