KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA, KILIMO NA MIFUGO YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA SHAMBA LA MBEGU KIBAHA.

0

Na. Edith Masanyika, Pwani

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo leo tarehe 19 Machi, 2024 imehitimisha ziara yake ya siku mbili jiijini Dar es Salaam kwa kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za shamba la mbegu na malisho la vikuge – Kibaha.

Shamba la malisho ya Vikuge linalomilikiwa na Wizara ya MIfugo na Uvuvi chini ya Idara ya Uendelezaji Nyanda za Malisho na Rasilimali na Vyakula na Mifugo lipo katika kijiji cha Vikuge kata ya Soga Wilaya ya Kibaha Pwani.

Lengo kuu la shamba hili ni kuzalisha mbegu za malisho kwa ajili ya kuwauzia wafugaji na wakulima wa malisho pamoja na kuzalisha malisho na kuwauzia wafugaji ili kuongeza upatikanaji wa malisho hayo pamoja na kutoa elimu na kuwajengea uwezo wafugaji kuhusu namna bora ya kuzalisha na kuhifadhi malisho.

Kamati ilipata wasaa wa kukagua shamba hilo na kujionea ukulima wa majani ya malisho pamoja na uzalishaji wa mbegu za malisho unavyoendelea na kupongeza kwa hatua hiyo nzuri ambayo inaleta tija katika suala zima la malisho ya mifugo katika Taifa letu.

Aidha, pongezi nyingi zilitolewa na Mheshimiwa Mwenyekiti pamoja na Waheshimiwa wajumbe kwa kazi nzuri iliyofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuwasihi kuendelea kutoa ujuzi huu wa ukulima wa malisho ya mifugo katika Mikoa mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *