MADEREVA WAASWA KUPUNGUZA MWENDOKASI WAWAPO NDANI YA HIFADHI YA MIKUMI
Watumiaji wa Vyombo vya moto wametakiwa kupunguza mwendokasi zaidi pindi wanapopita kwenye Hifadhi ya taifa ya mikumi ili kuepuka kugonga wanyama na kusababisha hasara kubwa ya kukosa fedha kutokana na utalii unaofanyika kwenye Hifadhi hiyo.
Hayo yamesemwa Februari 19,2024 na kamishna mkuu Msaidizi wa hifadhi ya Taifa Mikumi Kamanda ,Augustine Masesa wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ofisi za Makao makuu ya Hifadhi hiyo zilizopo mikumi mkoani Morogoro.
Kamanda Masesa Amesema pamekuwepo na changamoto kubwa ya wanyama kugongwa kutokana na mwendo kasi wa magari yanayokatisha kwenye Hifadhi hiyo licha kuwataka kutembea mwendo mdogo lakini wanakwenda mwendokasi kwa kufanya hivyo inasababisha madhara ya mara Kwa mara Kwa wanyama wetu
“Kama shirika ama Hifadhi Sasa tunafikiria kufunga kamera (CCTV) katika Hifadhi hii ya mikumi ili kudhibiti na kubaini wanaokwenda Kwa spidi kubwa kwani tunaamini kufanya hivi kutaokoa wanyama wetu kuwa salama zaidi.”Amesema
Pia katika hatua nyingine Kamanda Masesa ametoa rai Kwa watanzania na hasa kupitia nyakati za sikukuu mbalimbali na likizo kujitokeza na kutembelea Hifadhi ya taifa ya mikumi ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo hususani wanyama kama Simba , tembo,Swala,chui,viboko,mamba ikiwa sehemu ya Kukuza utalii wetu
Amesema hakuna mahala kwingine unaweza kuona wanyama hao Kwa ukaribu zaidi ya Hifadhi ya taifa ya mikumi hivyo nivema tukajenga tabia ya kutembelea na si kuwaachia wageni tu japo katika siku za hivi karibuni pamekuwepo na ongezo la watalii wa ndani kutembelea Hifadhi hiyo.
Pia akizungumzia royal tour ambayo ilizinduliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwanza Amesema wanamshukuru sana kiongozi huyo mkuu wa nchi kwani imeleta chachu na matunda yake yanaonekana kwani watalii wameongezeka ukilinganisha na huko nyuma .
Masesa Amesema watalii wengi ambao wanakuja kutembelea Hifadhi ya taifa Mikumi wanatoka Zanzibar Asubuhi na Ndege na kufika Hifadhi ya mikumi baada ya kutalii jioni wanarudi kulala Zanzibar hali ambayo kama Hifadhi inawapa hamasa Sasa ya kukaribisha wawekezaji ili kujenga hoteli kubwa za nyota tano ili watalii waweze kulala hifadhini pindi wanapokuja kutalii.
Aidha Amesema wanaendelea kuimarisha miundombinu na zaidi ujenzi wa kiwanja cha ndege ili Kuruhu ndege kubwa kutua na kuongeza idadi kubwa ya watalii lakini Kwa kifupi royal tour imelipa na mambo yanakwenda vizuri .
“Kikubwa watanzania waendelea kuja kutembelea vivutio vyetu na Kwa musimu huu wa sikuku ya pasaka basi watumie fursa hii kuja na watapata huduma zote ndani ya Hifadhi ikiwemo sehemu za maradhi, chakula , lakini Kuna utalii wa michezo na kubwa zaidi na chautofauti wataona wanyama Kwa karibu zaidi.”Amesema