RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:
- Amemteua Dkt. Thomas Nestory Bwana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Bwana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Mazingira (Biodiversity Conservation) Ofisi ya Makamu wa Rais. Anachukua nafasi ya Dkt. Geofrey Mkamilo ambaye amemaliza muda wake.
- Amemteua Abdul-Razaq Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Kabla ya uteuzi huu Bw. Badru alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB). Aidha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba atapangiwa kazi nyingine.
- Amemteua Dkt. Bill Kiwia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Dkt. Kiwia anachukua nafasi ya Bw. Badru ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Uteuzi huu unaanza tarehe 06 Februari, 2024