POLISI NA IPSEC NA SIMBA CYBER WAJA NA MWAROBAINI MAKOSA YA KIMTANDAO
Jeshi la Polisi Nchini Kwa kushirikiana na Kampuni ya IPsec ya nchini Israel na Simba Cyber ya nchini Tanzania wamekuja na mkakati wa kupambana na uhalifu mtandaoni.
Akizungumza katika mafunzo hayo naibu kamishna wa Polisi DCP Flugence Ngonyani ambaye aliongea Kwa niaba ya kamishna wa Uchunguzi wa kisayansi CP Shaban Hiki amesema mafunzo hayo yamejenga uelewa Mkubwa katika matumizi ya Tehama na uchunguzi wa Makosa ya Kimtandao kutoka Kwa wataalam hao wa Israel na Tanzania.
Ameongeza kuwa Kwa sasa Wahalifu wengi wamehamia katika mitandao huku akibainisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na wataalam wa ndani na nje ya nchi ilikubadilishana ujuzi katika usalama na uhalifu mitandaoni.
Pia ameishukuru kampuni hiyo Kwa kukubali kuendelea kuwezesha mafunzo hayo Kwa Jeshi la Polisi ili kuwajengea uwezo wa ubobezi katika uchunguzi wa Makosa ya kimtandao.
Kwa upande wake Mkurungenzi wa Simba Cyber ya nchini Tanzania Bw. Dan Shaham amesema wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu wa Kimtandao hapa nchini.
Nae Mratibu wa wataalam hao kutoka Israel mrakibu wa Polisi SSP Georgina Matagi licha ya kushukuru amesema Jeshi hilo litaendelea kuwatumia marafiki wake wa nje na ndani ya Tanzania katika kubadilisha uzoefu na ujuzi wa mapambano ya uhalifu wa kimtandao ambao unahitaji mtaji mkubwa wa wataalam wa Tehema.