WANANCHI WAKOMBOLEWA KWA MRADI WA MAJI WA MILIONI 292

0
0T9A4527

Mbunge wa Jimbo la Kondoa ambae pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amefanya uzinduzi  wa mradi wa maji uliogarimu kiasi cha shilingi million 292 katika kijiji cha kwadelo kilichopo Wilaya ya Kondoa  kata ya kwadelo, ulio tekelezwa  na kampuni ya Serengeti  Breweries
Katika uzinduzi huo Waziri Ashatu amesema mradi huu wa maji umetatua changamoto kubwa ya maji iliokua ikiwasubumbua wananchi na kuhatarisha maisha yao kwakufwata maji umbali mrefu hususani wanawake.

Pia Katika hotuba yake Waziri Ashatu  amewataka wananchi  kuutunza mradi huo na nijukumu la kila mtu kuutuza kuanzia kwenye vyanzo vya maji  ili uzidi kusaidia  kizazi cha sasa na vijavyo.

Aidha ameitaka kampuni ya Serengeti  breweries kuendelea kuwa saidia wananchi  wa kondoa kwa kuwa ongezea mradi mwingine wa maji ambao utasaidia kutatua chanagmoto ya maji kati baadhi ya maeneo yalio baki
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Serengeti  breweries Dkt. Obinna Anyalebechi  amewashukuru wanachi  wa kwadelo kwa ushirikiano mkubwa walio utoa katika kukamilisha mradi huu na amewataka kushirikiana kuutunza mradi huo  kwa manufaa yao na kijiji.

Meneja  wa Ruwasa  Mkoa wa Dodoma Bw. Mbaraka Rajabu amesema lengo la serikali kupitia Ruwasa ni kuhakikisha  uboreshaji wa miundombinu ya maji na kuhakikisha wananchi wote wanapa huduma ya maji kwa uraisi

default

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *