MENEJIMENTI YA NHC YAKAGUA MAENDELEO YA UENDELEZAJI SAFARI CITY ARUSHA

0
503557187_1286725589673298_9110051491471587815_n.heic

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bw. Hamad Abdallah, ametembelea Safari City jijini Arusha kukagua maendeleo ya uendelezaji wa eneo hilo linalopakana na Barabara ya Afrika Mashariki na Uwanja mkubwa wa michezo unaotarajiwa kutumika kwenye mashindano ya AFCON.

Safari City ni mji wa kisasa uliopangwa na NHC, ambapo wananchi wameuziwa viwanja vya makazi, biashara na huduma – ikiwa ni sehemu ya kutoa fursa kwa kila Mtanzania kumiliki ardhi iliyopimwa na kuendelezwa kwa viwango bora.

Miundombinu ya barabara, umeme, maji na huduma za kijamii inaendelea kuwekwa kuhakikisha eneo hili linakuwa kitovu cha makazi na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa Kanda ya Kaskazini.
#UhondoTVUPDATES

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *