KATIBU MTENDAJI WA TUME YA MADINI AHIMIZA UBUNIFU, WELEDI KWA WATUMISHI

0
IMG-20250623-WA0006

KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Nsajigwa Kabigi, wametembelea banda la Tume ya Madini katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayohitimishwa leo katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo, viongozi hao wamejionea namna Tume ya Madini inavyoshiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake, huduma mbalimbali zinazotolewa na mafanikio yaliyopatikana katika usimamizi wa rasilimali za madini nchini.

Mhandisi Lwamo sambamba na kuwapongeza wataalam waliopo kwenye banda hilo, amewataka kuendelea kutoa huduma kwa weledi, uwazi na ubunifu kwa kuzingatia mabadiliko ya kidijitali ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa kwa haraka na kwa usahihi.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji”, ambayo inalenga kuimarisha utendaji katika utumishi wa umma kupitia matumizi ya teknolojia.

Maadhimisho haya yanahitimishwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), ambapo taasisi mbalimbali za serikali zimepata fursa ya kuonesha huduma wanazotoa na jinsi zinavyowahudumia wananchi kwa uwazi, uwajibikaji na ubunifu.

Tume ya Madini imeendelea kuwa taasisi muhimu katika kukuza uchumi wa nchi kupitia usimamizi endelevu wa Sekta ya Madini, huku ikiendelea kuboresha huduma kwa kutumia mifumo ya kidijitali kwa maendeleo jumuishi ya Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *