NHC YAKUTANA NA KAMATI YA WAPANGAJI KUJADILI MAENDELEO YA MAKAZI MAPYA

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limefanya kikao maalum na Kamati ya Wapangaji na Wamiliki wa zamani wa nyumba zilizobomolewa, kwa ajili ya kujadili mwenendo wa ujenzi mpya wa makazi ya kisasa unaotekelezwa kwa mfumo wa ubia.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Wapangaji, Bw. Shafiq Mohamed, ambapo wamejadili kwa kina masuala muhimu ya maslahi ya pande zote mbili.


Ujenzi mpya wa nyumba hizi ni sehemu ya mkakati wa NHC wa kubadilisha sura ya maeneo ya zamani na kuyaendeleza kwa majengo ya kisasa, salama na yenye huduma bora zaidi. Wamiliki wa zamani wameendelea kushirikishwa kwenye mchakato huo kwa misingi ya haki na usawa.
Mazungumzo yameenda vizuri kwa hali ya maelewano, dhamira ya kweli na maono ya pamoja katika kuhakikisha kuwa kila mdau ananufaika na mabadiliko haya ya kimkakati.