RC HOMERA AITAKA NHC KUWEKEZA KWENYE MAENEO YA BIASHARA MBEYA

0
500586960_1236777324626971_4713636140541657385_n.heic

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Juma Zuberi Homera amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kufanya uwekezaji wa nyumba za kupangisha, hoteli au maduka ya kisasa (shopping malls) katika maeneo yaliyowazi jijini Mbeya hususani eneo la Soko la Zamani ambapo yanafanyika maonyesho ya Wafanyabiashara Mbeya.

Akizungumza katika banda la Shirika la Nyumba la Taifa wakati wa Maonyesho ya Mbeya City Expo Dr. Homera amesema, “Shirikianeni ninyi na jiji, mnajenga hapa appartments za kutosha, mnaweza mkajenga shopping mall kubwa hapa. Kama mtashindwa Mkuu wa Mkoa ana eneo, pale Mwanjelwa kuna eka sita linataka muwekezaji.” Alisema Dr. Homera

Afisa Mauzo Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Ndg, Daniel Kure amebainisha miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na NHC na kuwataka wadau wa ujenzi kushirikiana na Shirika hilo.

“Katika maonyesho haya tumewaletea miradi inayoendelea na inayotarajia kuuanza. Mradi unaoendelea sasa ni mradi wa Kawe 711 kule Dar es Salaam, ni mradi wa makazi wenye vyumba vitatu, vyumba viwili na vyumba vinne lakini pia tuna mradi wa Samia Housing scheme ambao unakuja awamu ya pili utakuwa na vyumba viwili, vitatu na kimoja.” Alisema

Aidha Kure amesema Shirika la Nyumba la Taifa limeanza kushirikiana na wadau wa ujenzi katika maeneo ya Mbeya, Dar es Salaam na mengine hivyo ni fursa kwa wadau hao kufika katika banda la NHC ili kupata uelewa wa mambo mbalimbali yanayofanywa na NHC. 📢 WITO:
Wadau wa ujenzi na wawekezaji wote, tembeleeni banda la NHC kwenye Mbeya City Expo 2025 kwa taarifa, fursa na ushirikiano wa kimaendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *