WANANCHI HANDENI  WAIPONGEZA REA KWA USAMBAZAJI WA MITUNGI YA GESI YA KILO SITA KWA BEI YA RUZUKU

0
IMG-20250524-WA0013

Wananchi wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga waipongeza REA kwa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku.

Mitungi hiyo inasambazwa kila wilaya kwa bei ya ruzuku ya shillingi 17,500 na kila wilaya  idadi ya mitungi 3,255 kusambazwa.

Usambazaji wa mitungi hiyo, unaunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia suluhu Hassan, ya kuhakikisha mpaka ifikapo mwaka 2034 asilimia themanini (80) ya watanzania wawe wanatumia Nishati safi ya kupikia.

Mitungi hiyo inasambazwa kwa bei ya ruzuku ili kumuwezesha kila mtanzania wa hali  yoyote kuwa na uwezo wa kutumia Nishati nishati safi na salama ya kupikia.

Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dk. Samia suluhu Hassan kupitia REA imetoa kiasi cha shilingi milioni 455.7 ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huu wa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo kwa bei ya ruzuku 26,040 mkoani Tanga.

Serikali inatamani kuona kila mtanzania wa hali yoyote, Mahali popote na jinsia yoyote katika maeneo ya vijijini anakuwa na uwezo wa kutumia Nishati safi na salama ya kupikia na kuachana na matumizi ya nishati chafu.

Naye msimamizi wa mradi Kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mkomi amesema serikali kupitia REA imetoa kiasi hicho kikubwa cha pesa ili kufanikisha utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku mkoani Tanga ukiwa na lengo madhubuti la kuhakikisha ustawi wa maisha ya wananchi una imarika katika nyanja zote za kijamii, kiafya, usawa wa kijinsia, uchumi, Mazingira pamoja na mabadiliko ya tabia Nchi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *