WIZARA YA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YALIOMBA BUNGE BAJETI YA BILIONI 291.5

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/26 jijini Dodoma leo Mei 14, 2025. Silaa ameliomba Bunge lipitishe bajeti ya wizara hiyo jumla ya Shilingi Bilioni 291,533,139,000 ikiwa na vipaumbele vifuatavyo;
i. Kutunga, kuhuisha na kusimamia
utekelezaji wa miongozo inayosimamia Sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
ii. Kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu na Posta kote nchini.
iii. Kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kukuza na kuimarisha Biashara Mtandao Nchini.
iv. Kuimarisha miundombinu
itakayowezesha utekelezaji wa uchumi wa kidijitali.
v. Kuimarisha ulinzi na usalama wa
anga ya mtandao; na
vi. Kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuchochea ubunifu na kuimarisha ustawi wa kampuni changa (Startups).