BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA UCHUKUZI KWA KISHINDO

0
20250515_154115

Bunge la Tanzania limepitisha Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi ya Shilingi Trilioni mbili, Bilioni mia saba arobaini na sita, Milioni mia nne themanini na tano na kumi na nane elfu (2,746,485,018,000) kwaajili ya matumizi ya mwaka 2025/26.

Wakati wa hitimisho la Mjadala wa Bajeti hiyo, Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewashukuru Wabunge wote 15 waliochangia Mjadala wa Bajeti hiyo kwa njia ya kuzungumza na maandishi, akiahidi kwamba Wizara yake itayafanyia kazi maoni, mapendekezo na ushauri uliotolewa, ikiwemo kuondoa tatizo la kuchelewa kwa safari za ndege zenye kuendeshwa na Shirika la ndege la Tanzania ATCL.

Awali Wizara hiyo pia imebainisha kwamba kwa mwaka ujao wa fedha, pamoja na mambo mengine itaendeleza ujenzi wa reli ya kisasa SGR katika ushoroba wa kati, kununua vitendea kazi pamoja na kuboresha reli zilizopo, kuifanyia maboresho ATCL, kuboresha miundombinu na huduma za bandari pamoja na kuendeleza ujenzi wa meli mpya na maboresho ya viwanja vya ndege na Meli zilizopo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *