BENKI YA AZANIA YAKABIDHI MADAWATI 200 KWA SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI MUSOMA

0
IMG-20250502-WA0155

Benki ya Azania imekabidhi jumla ya madawati 200 kwa ajili ya Shule za Sekondari na Msingi wilayani Musoma kwa lengo la kuunga juhudi zinazofanywa na serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi madawati katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo Elizabeth Koboko Meneja wa Benki ya  Azania Tawi la Serengeti amesema kuwa madawati hayo ni sehemu ya gawio kwenye jamii kutokana na faida iliyopatikana kwa kipindi cha mwaka mzima.

“Kwa kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuinua kiwango cha elimu nchini, leo hii tunakabidhi viti na meza 200. Benki ya Azania imeguswa na uhitaji wa meza na viti uliopo kwenye shule za Sekondari katika Manispaa ya Musoma ijapokuwa Serikali imejitahidi kutatua kwa kiasi kikubwa.

Sisi kama taasisi ya fedha tumeona tunalo jukumu la kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi katika sekta ya Elimu, hivyo tulipoona fursa ya kuwashika mkono tukafanya hivyo bila kusita ikizingatiwa kuwa Benki ya Azania ni moja ya Benki ambazo hurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii (CSR) kupitia sekta mbalimbali, tunaamini vifaa hivi vitakwenda kuchangia kupunguza ukubwa wa changamoto ya upungufu wa viti na meza iliyokuwepo katika Manispaa yetu ya Musoma na sasa kiwango cha ufaulu kitaongezeka”.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika zoezi hilo ameishukuru Benki ya Azania kwa kutambua jamii inahitaji gawio kupitia taasisi za elimu hasa kupunguza wimbi la wananfunzi kukaa chini kutokana na upungufu wa madawati.

Aidha Kanali Mtambi amepiga marufuku kwa mwanafunzi wa mkoani Mara kukutwa amekaa chini kwa kisingizio cha upungufu wa madawati shuleni kwani Serikali imejitahidi kuboresha miundombinu ya wananfunzi pia na taasisi mbalimbali zinazotambua umuhimu wa elimu ikiwemo na Benki ya Azania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *