WAZIRI MAVUNDE ASHUSHA UZI WA MAFANIKIO YA SEKTA YA MADINI MIAKA MINNE YA RAIS. DKT. SAMIA

0
IMG-20250425-WA0003

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameeleza mafanikio makubwa ya Sekta ya Madini chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha uwepo madarakani na kupelekea mchango wa Sekta kufikia asilimia 10.1 mwaka 2024 mwaka mmoja kabla lengo lilowekwa.

Ameeleza mafanikio hayo leo Aprili 24, 2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza katika Programu ya Kurasa 365 za Mama iliyoratibiwa na Clouds Media kwa kushirikiana na Wizara ya Madini.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kutuongezea Bajeti ya Wizara ya Madini kutoka shilingi bilioni 89 mwaka wa fedha 2023/24 hadi kufikia shilingi bilioni 231 kwa mwaka huu wa 2024/25 ambako Fedha nyingi zimeelekezwa kwenye Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kuimarisha shughuli za utafiti wa kina wa madini ambayo ndio uti wa mgongo wa Sekta hii” amesema Mavunde

BAADHI YA DONDOO ZA MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA MADINI ZILIZOAINISHWA NA WAZIRI MAVUNDE

◇ Kuongezeka kwa mchango wa Sekta kutoka asilimia 7.2 mwaka 2022 hadi 9.0 mwaka 2023 na kufikia asilimia 10.1 mwaka 2024 kabla ya lengo lililowekwa kwenye Sera ya Madini ya mwaka 2009 nna Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.

◇ Sekta imechangia Asilimia 56.2 ya mauzo yote nje ya nchi kupitia biashara ya madini huku Mapato ya kodi ndani ikiwa ni shilingi trilioni 2.1 ikiwa ni zaidi ya asilimia 15 ya kodi ya ndani.

◇ Mwaka wa fedha 2015/16 sekta hii ya madini ilikusanya shilingi bilioni 162 pekee, mwaka 2023/24 sekta ilikusanya shilingi bilioni 753.82 na mwaka huu wa 2024/25 tayari kiasi cha shilingi bilioni 833 kufikia leo Aprili 24, 2025.

◇ Ajira rasmi katika Sekta ya Madini ndani ya kipindi hicho cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia madarakani imefika 19,356 sawa ambako asilimia 97.4 ni Watanzania bado ajira zisizo rasmi.

◇ Tumeanzisha Masoko 43 na vituo vya ununuzi wa madini 109 na Jumla ya mzunguko wa fedha katika masoko hayo umefikia shilingi trilioni 2.2 na kuwapa wachimbaji wadogo uhakika wa soko na bei nzuri.

◇ Tumefanikiwa kurejesha minada wa madini ya vito ya ndani na ya kimataifa na tayari imeshafanyika Mirerani na Arusha na kuleta manufaa pamoja na tija.

◇ Kuendeleza wachimbaji wadogo, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo kuongeza mitambo ya uchorongaji ilikwepo mitano sasahivi imekuja mengine 10 kwa ajili ya kuwasaidia wachimbaji wadogo, vijana na wanawake, maeneo ya uchimbaji n.k

◇ Tumeanzisha utaratibu wa kuwatambua wachimbaji wadogo wote ili tuweza kuwasaidia kwa utaratibu maalum.

◇ Maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia ni kuhakikisha watanzania wanajengewa uwezo wa kuendesha shughuli za uchimbaji madini na kushiriki kwa wingi na kwa tija.

◇ Tunataka wachimbaji wetu wadogo wafaulu (graduate) kutoka kuwa wachimbaji wadogo na kuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa.

◇ Ununuzi wa madini ya dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuimarisha akiba ya fedha za kigeni pamoja na sarafu yetu ni hatua kubwa na ya kipekee.

◇ BoT mpaka hivi sasa imenunua tani 3.1 kati ya lengo la tani 6 Tukifika mwezi wa 7 tutakuwa tumeingia katika 10 bora ya nchi zenye hifadhi kubwa ya dhahabu barani Afrika ndani ya muda mfupi tangu mchakato huo kuanza mwezi Oktoba 2024.

◇ Kuendelea kuwezesha taasisi zilizopo chini ya Wizara Stamico kumiliki mgodi mkubwa wa mfano hapa nchini na pia wanajenga kiwanda cha kusafisha madini ya chumvi ili kuwasaidia wakulima wa chumvi nchini kupata uhakika wa soko, Tume ya Madini, GST tunanunua helicopter kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina wa kijiolojia pamoja na Ujenzi wa maabara ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi wa sampuli za madini.

◇ Miaka minne uwekezaji umeongezeka nchini Tanzania kutokana na mazingira rafiki ya uwekezaji hapa nchini chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia

◇ Tumetoa leseni kubwa katika miradi kadhaa ikiwemo wa madini tembo (Heavy Mineral Sands) uliopo ebeo la tajiri Mkoani Tanga

◇ Tuna gesi ya helium yenye ubora mkubwa zaidi duniani kule Songwe na Rukwa, na kutuweka kwenye nafasi ya kipekee ya ugavi wa rasilimali hiyo pindi uzalishaji wake utakapoanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *