MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS SAMIA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTAMADUNI NA MICHEZO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Aprili 22, 2025 anamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kikao kazi cha 15 cha Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo Tanzania.
Kikao hicho cha Mafundo na Mazingativu kinalenga kujadili maendeleo ya sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Pia kikao hicho kinatoa nafasi kwa washiriki kujadili fursa za sekta, kubaini changamoto zinazoikabili sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo na kupendekeza njia za utatuzi wa changamoto hizo.



