SERIKALI KUTUMIA TRILIONI 1.18 UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA ZA WILAYA

0
IMG-20250416-WA0041

Katika mwaka wa fedha 2025/26, Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini TARURA imepanga kutumia shilingi trilioni 1.18 kwa ajili ya ujenzi, matengenezo, ukarabati wa miundombinu ya barabara na usafiri na usafirishaji wa vijijini na mijini.

Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 257.03 ni za Mfuko wa Barabara, shilingi bilioni 127.50 Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, shilingi bilioni 325.77 ni za tozo ya mafuta ya petroli na dizeli ya shilingi 100 kwa lita na shilingi bilioni 423.79 ni fedha za nje.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 jijini Dodoma.

Amesema kupitia Mfuko wa Barabara, fedha hizo zitaenda kutekeleza matengenezo na ukarabati wa barabara za wilaya zenye urefu wa kilomita 23,105.78, box kalavati 23, mistari ya kalavati 1,647, Drift 2, na mifereji ya maji ya mvua mita 73,405, barabara za lami kilometa 17, barabara za changarawe kilometa 108.8 na madaraja 2.

Aidha, ujenzi wa kilometa 91.97 kwa kiwango cha lami, kilometa 2,621.40 za changarawe, madaraja 85, box kalavati 91, mitaro ya maji ya mvua mita 10,989 drifti tano (5), mistari ya kalavati 666 na taa za barabarani 345 zitatekelezwa kupitia Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.

Ameongeza kuwa kupitia tozo ya mafuta ya petroli na dizeli ya shilingi 100 kwa lita, fedha hizo zitatekeleza ujenzi wa km 252.42 kwa kiwango cha lami, kilomita 6,939.41 za changarawe, madaraja 51, box kalavati 336, mistari ya kalavati 1,719, Drift 2, na mifereji ya maji ya mvua mita 63,836.

Mhe. Mchengerwa amesema ujenzi wa barabara za lami Km 147.50, ujenzi wa mifereji ya maji ya
mvua mita 24,600, ujenzi wa masoko 9, ujenzi wa stendi kuu 4
za mabasi na stendi ndogo 2 pamoja na ujenzi wa maghala 2
ya kuhifadhia mazao kwenye miji 12 ya Fungu la Kwanza la Mradi wa TACTIC unaendelea.

Pia kuanza kwa ujenzi kwenye Halmashauri za Miji 15 za Fungu la Pili la Mradi wa TACTIC pamoja na kukamilisha mchakato wa maandalizi ya
Mradi wa TACTIC Fungu la Tatu katika
Halmashauri za Miji 18.

Amesema ujenzi wa barabara Km 33 kwa kiwango cha lami katika halmashauri za Wilaya za Iringa (Wenda-
Mgama kilomita 19) na Mufindi (Mtili-Ifwagi
kilomita 14) unaendelea, pmoja na kuanza kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Km 33 katika halmashauri za Wilaya za Handeni, Ruangwa na Mbogwe kupitia mradi wa RISE.

Vilevile, uboreshaji wa Bonde la Msimbazi lenye Hekta 5.7, ujenzi wa karakana ya mabasi
ya mwendo kasi katika eneo la Ubungo
Maziwa, ujenzi wa tuta kilomita 6.7 katika eneo la Bonde la Mto Msimbazi, ujenzi wa Bohari Mpya ya BRT eneo la Ubungo Maziwa, ujenzi wa miundombinu ya barabara awamu ya kwanza zenye jumla ya
kilomita 132 katika Manispaa za Kinondoni,
Ubungo, Temeke, Ilala na Kigamboni.

Pia, ujenzi wa miundombinu ya
barabara awamu ya pili ya Mradi wa DMDP
zenye urefu wa kilomita 118 kiwango cha
lami katika Manispaa za Kinondoni, Ubungo,
Temeke, Ilala na Kigamboni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *