BENKI YA AZANIA YADHAMINI MKUTANO WA TAWIFA 2025

Benki ya Azania imepata heshima kuwa mdhamini wa Mkutano wa Wanawake katika Sekta ya Fedha Tanzania (TAWIFA) 2025, uliofanyika chini ya kauli mbiu: “Wekeza kwa Wanawake, Chochea Maendeleo.”
Mkutano huu mkubwa ulifunguliwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu, Mh. Dkt. Doto Biteko. Kupitia ushiriki wake, Benki ya Azania ilipata nafasi ya kuonyesha juhudi zake katika kuwawezesha wanawake kifedha kupitia bidhaa na huduma zake bunifu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania alitoa hotuba kuu, akisisitiza umuhimu wa ujumuishaji wa kifedha na faida za moja kwa moja kwa taasisi zinazowekeza kwa wanawake.

